Japan yajutia vita vya dunia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Japan yajutia vita vya dunia

Emperor Akihito wa Japan ameelezea kujutia kwake kutoka na vita vya pili vya dunia kwenye sherehe za kuadhimisha miaka 70 tangu nchi yake ijiondoe kutoka kwa vita hivyo.

Amesema kuwa unyama uliofanyika wakati huo hautarudiwa tena.

Maelfu ya watu wanatoa heshima zao katika makaburi yenye utata yanayoonekana na majirani wa Japan kuwa ishara ya dhuluma zake vitani.

Shirika la habari la taifa la Japan linasema kuwa waziri mkuu Shinzo Abe ametuma toleo lake kwa makaburi yenye utata lakini hakuhudhuria binafsi.

Kusalimu amri kwa Japan kuliinusuru korea kusini kutoka miaka 35 ya kutawaliwa. Siku ya Ijumaa Abe alijutia taabu zilizosababishwa na Japan kote eneo hilo.