Pigo kwa mapatano Sudan Kusini

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Pigo kwa mapatano Sudan Kusini

Matumaini ya kuafikiwa makubaliano ya amani ya kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan Kusini yamepata pigo kubwa kufuatia tangazo kuwa rais hatahudhuria mazungumzo yaliyopangwa pamoja na waasi.

Msemaji wa rais Salva Kiir alisema kuwa hawezi kuhudhuria mazungumzo katika mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa wikendi hii.

Amesema kuwa serikali haijajiondoka kwenye mazungumzo na waasi wanaongozwa na Riek Machar na badala yake makamu wa rais ataenda Ethiopia.

Wapatanishi wameweka hadi Jumatatu ili kukamilika kwa makubaliano ya kumaliza mapigano ambayo yamewalazimu karibu watu milioni mbili kuhama makwao.