Al-Maliki aweza kushtakiwa

Nuri al-Maliki, waziri mkuu wa zamani wa Iraq Haki miliki ya picha REUTERS

Uchunguzi rasmi uliofanywa nchini Iraq umekuta kuwa waziri mkuu, Nouri al-Maliki, na wanasiasa na wanajeshi kama 30 wa daraja za juu, wanabeba dhamana kwa mji wa Mosul kutekwa na wapiganaji wa Islamic State mwaka jana.

Spika wa bunge la Iraq amesema ripoti hiyo iliyotayarishwa na kamati ya bunge itapelekwa kwa mkuu wa mashtaka ili kuanzisha hatua za kisheria.

Saa chache kabla waziri mkuu, Haider al-Abadi, alitoa idhini kwa mahakama ya kijeshi kusikiliza kesi za makamanda wa jeshi walioondoka vitani wakati mji wa Ramadi ulipotekwa na IS mwezi May mwaka jana.