Wafuasi wa Dadis Kamara wakabiliwa Guinea

Haki miliki ya picha
Image caption Moussa Dadis Camara

Polisi nchini Guinea wamepambana na wafuasi wa aliyekuwa kiongozi wa kijeshi wa nchi hiyo Moussa Dadis Camara.

Takriban watu 2000 walikuwa wamekusanyika katika uwanja wa ndege kwenye mji mkuu wa Conakry kufuatia uvumi kwamba bwana Camara angerejea nyumbani kutoka uhamishoni.

Wengi waliondoka baada ya saa kadhaa lakini kundi dogo lilikataa kuondoka.

Bwana Camara amesema kuwa ana nia ya kuwania urais ambao unapangiwa kufanyika mwezi Oktoba licha ya kuhukumiwa mwezi uliopita kwa kuhusika kwenye mauaji ya zaidi ya waandamanaji 156 miaka sita iliyopita.