Wahamiaji wanaoingia Uingereza wapungua

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wahamiaji wanaoingia Uingereza wapungua

Kampuni inayosimamia barabara za reli za chini kwa chini kati ya Uingereza na Ufaransa inasema kuwa kumekuwa na kupungua kwa idadi ya wahamiaji wanaojaribu kuingia katika barabara hizo katika bandari wa Calais.

Kampuni hiyo ya Euro Tunnel inasema kuwa karibu wahamiaji 150 hujaribu kutumia njia hizo kila siku kwa lengo ya kuingia nchini uingereza.

Mwezi uliopita karibu wahamiaji 2000 walijaribu kutumia njia hizo. Kampuni hiyo inasema kuwa kupungua kwa watu hao kunatokana na kuwepo polisi zaidi na kuwekwa ua mpya.