Je,kampuni ya Apple inatengeza gari?

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Apple

Uvumi kwamba kampuni ya Apple huenda inajiandaa kuanzisha utengezaji wa magari umekuwa ukienea kana kwamba mashabiki wa Apple wamekuwa wakitarajia kitu kipya kutoka kwa kampuni hiyo.

Kufikia sasa kumekuwa na mitindo ya aina ya gari hilo bila ushahidi wowote kwamba kuna kitu kinakuja.

Lakini sasa kuna thibitisho:Gazeti la The Gurdian limezungumza na muhandisi wa kampuni ya Apple Frank Fearon na maafisa kutoka kwa kiwanda kimoja cha kukagua magari GoMentum.

''Tunataka kuelewa mda na nafasi iliopo na vile tutakavyo ratibu watakaoitumia,gazeti hilo limemnukuu Fearon akiandika.

Taarifa hiyo ilitumwa mnamo mwezi Mei.Kituo cha GoMentum kiko Concord,mji ambao utakuchukua mda wa dakika 30 iwapo utakuwa ukiendesha gari kaskazini mashariki mwa mji wa San Fransisco.

Swali ni barua hiyo iansema kuhusu harakati za Apple za kutaka kutengeza gari?,Hadi kufikia sasa tunajua kwamba Apple imewaajiri wataalam kadhaa wa magari ambao wanadaiwa kusimamia mradi kwa jina Titan ijapokuwa hilo halijathibitishwa na Apple.

GoMentum wako chini ya masharti makali kwamba hawafai kutangaza makubaliano ya mradi huo,lakini walithibitisha kwa Guardian kwamba 'wanavutiwa'