Walio na kisukari waongezeka Uingereza

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Walio na kisukari waongezeka Uingereza

Idadi ya watu wanaoishi na ugonjwa wa kisukari imepanda kwa karibu asilimia 60 katika kipindi chaa muongo mmoja uliopita kwa mujibu wa shirika moja nchini Uingereza.

Shirika la Diabetes UK, linasema kuwa zaidi ya watu milioni 3.3 wana aina fulani ya ugonjwa wa kisukari ambalo ni ongezeko kutoka watu milioni 2.1 mwaka 2005.

Kutokuwa na uwezo wa kudhibiti viwango vya sukari kwenye damu inaweza kusababisha mtu kuwa kipofu au kukatwa miguu.

Haki miliki ya picha SPL
Image caption Walio na kisukari waongezeka Uingereza

Karibu visa vyote vya ugonjwa wa kisukari vilivyoripotiwa ni vya aini ya pili au type 2 diabetes ambao husababishwa na kutokula kwa njia nzuri na uzito mkubwa wa mwili.

Barbara Youg ambaye ni mkurugenzi mkuu wa Diabetes UK amesema kuwa serikali inahitaji kuchukua hatua kuzuia visa vipya na kuboreha huduma matibabu kwa wale ambao tayari wana maradhi hayo.