Shughuli za kutafuta ndege zasitishwa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Shughuli za kufatuta ndege zasitishwa

Utawala nchini Indonesia unasema kuwa hali mbaya ya hewa imewalazimu kusitisha oparesheni za kuwatafuta manusura wa ajali ya ndege ambayo ilianguka siku ya Jumapili katika milima iliyo mashariki mwa Papua.

Ndege hiyo ilikuwa imebeba abiria 54 na karibu dola nusu milioni pesa taslimu.

Mkuu wa posta katika mji mkuu wa Papua wa Jayapura aliambia BBC kuwa pesa hizo zilizokuwa ndani ya mifuko minne ilikuwa sehemu ya mchango wa serikaki kwa watu maskini.

Shirika moja linalohusika na kusaka ndege hiyo linasema kuwa limegundua yaliyo mabaki ambao ni umblai ya kilomita 50 kutoka mahala ndege hiyo ilitakiwa kutua.