Dawa ya Lariam haifai kutumiwa jeshini

Haki miliki ya picha MOD
Image caption Dawa ya Lariam haifai kutumiwa jeshini

Wito umetolewa wa kutaka kusitishwa mara moja matumizi ya dawa inayokumbwa na utata ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa malaria ambayo hutumiwa na wanajeshi wa uingereza.

Athari zinazotokana na matumizi ya dawa ya Mefloquine au Lariam imehuziswa na mafadhaiko pamoja na matatizo mengi ya kiakili.

Mbunge wa Conservative Johnny Mercer anasema kuwa amepokea barua kadha kutoka kwa wanajeshi wanaodai kuwa wameathiriwa tangu waitumie dawa hiyo.

Image caption Mbunge Johnny Mercer anataka dawa kufanyiwa uchunguzi

Bwana Mercer ambaye ni mwanajeshi wa zamani aliyehudumu nchini Afghanistan anaitaka serikali iache kuwapa wanajeshi dawa hiyo hadi pale utafiti zaidi utakapofanywa.

Anasema kuwa amepata barua mara moja au mbili kwa wiki kutoka kwa watu kote kote nchini Uingereza ambao wameathiriwa au wanamfahamu mtu aliyeathiriwa baada ya kutumia dawa ya Lariam.

Dr Ashely Croft ambaye alikuwa mwanajeshi kwa miaka 27 amefanya uchunguzi mara mbili kuhusu dawa ya Mefloquine na anaamini kuwa theluthi moja ya wale hutumia dawa hiyo huathirika kwa njia moja au nyingine.