Mbabazi achukua fomu za kuwania urais Uganda

Haki miliki ya picha
Image caption Mbabazi achukua fomu za kuwania urais wa Uganda

Waziri mkuu wa zamani wa Uganda Amama Mbabazi amechukua fomu za kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Huyu ndio mtu wa kwanza kuchukua fomu hizo kutoka tume huru ya uchaguzi kuhusiana na uchaguzi mkuu wa hapo mwakani.

Sura ya kisiasa nchini Uganda ya wakati wa kipindi cha uchaguzi imeanza kujitokeza.

Hii ni baada ya wenye nia ya kuwania nafasi mbalimbali kuanza kujitayarisha kwa minajili ya uchaguzi huo.

Wa kwanza ni John Patrick Amama Mbabazi waziri mkuu wa zamani wa Uganda na aliyekuwa mshirika wa karibu wa miaka mingi wa rais Museveni hadi miezi kadhaa walipotofautiana na rais kumvua madaraka ya uwaziri mkuu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye

Mbabazi alichukua fomu jumatatu kutoka tume ya taifa inayohusika na uchaguzi.

Fomu alizochukua ni za uteuzi kama mgombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao mwaka wa 2016.

Mbabazi ambae pia aliwahi kuwa katibu mkuu wa chama tawala cha NRM kabla ya kutangaza nia ya kugombea kama mtu wa kujitegemea.

Hata hivyo anasema baado ni mwanachama wa chama tawala cha NRM ilhali chama hicho kina mgombea mmoja wa kiti hicho ambaye ni rais Museveni.

Museveni mbali na kuonyesha nia yake hajachukua fomu ya kuwania urais kutoka kwa tume ya uchaguzi.

Vyama vya kisiasa nchini havijatangaza rasmi mshika bendera wa vyama hivyo kimoja kimoja japo viliunda ushirika wa The Democratic Alliance-TDA- na kuahidi kuja na mgombea mmoja kupambana dhidi ya mgombea kutoka chama tawala cha NRM.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Museveni mbali na kuonyesha nia yake hajachukua fomu ya kuwania urais kutoka kwa tume ya uchaguzi.

Harakati za leo za kutoa fomu kwa wagombea urais katika uchaguzi mkuu ujao huenda zilikuwa za wale watakao simama bila kutegemea chama chochote.

Hii ni kwa sababu Mbabazi anaonekana anajitegemea.

Pia mwingine aliechukua fomu za uteuzi ni Prof Baryamureeba zamani akihudumu kama makamu mkuu wa chuo kikuu cha Makerere.

Image caption Wapinzani wakuu wa rais Museveni, Besigye na Mbabazi

Wengine wanaosubiriwa kutoa fomu ni Dr Kiiza Besigye, ambae hadi sasa anajipigia debe dhidi ya mkuu wa sasa wa chama cha upinzani cha FDC- Generali Mstaafu Mugisha Muntu, kati yake nani achaguliwe kama mshika bendera wa chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.

Aliekuwa makamu rais Dr Gilbert Bukenya naye wakati fulani alionyesha hamu ya kuwania kiti cha urais wa nchi..lakini hajajitokeza waziwazi kama hawa wanne- Museveni; Mbabazi, Prof Baryaamureeba, Kiiza Besigye pamoja na Mugisha Muntu.