Wamiliki wa Ghala hatiani China

Haki miliki ya picha BBC CHINESE

Chombo cha habari cha taifa la China kimetangaza kuwa ,wamiliki wawili wa ghala ambazo zilisababisha mlipuko mkubwa wiki iliyopita walipata kibali cha kuhifadhi bidhaa hizo zenye madhara kwa njia ya kujuana.

Wamiliki hao walipata kibali batili kinachowaruhusu kuwa na ghala hilo karibu na makazi ya watu wakati sheria hairuhusu.

shirika la habari la Xinhua,nchini China limesema kuwa mmoja wa wamiliki ni mtoto wa polisi mkuu wa zamani wa eneo hilo wakati mwingine alikuwa kigogo wa kampuni ya taifa ya kemikali .

Hata hivyo wamili wote wawili wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kusababisha mlipuko mkubwa uliosababisha vifo vya watu wapatao mia moja na kumi na wanne.