Ugiriki yapata afueni ya kiuchumi

Image caption Bunge la Ujerumani

Bunge la ujerumani limepitisha maamuzi ya kuikomboa Ugiriki kiuchumi kutokana na matakwa ya wengi licha ya kuwa na wasiwasi kuwa kansela Merkel angekutana na upinzani kutoka kwa chama chake.

Zaidi ya wabunge mia nne wamekubaliana na serikali na mia moja na thelathini wamepinga mpango wa kulilipa deni hilo la dola bilioni tisini na nne.

Waziri wa fedha ,wolfgang Schauble alipendekeza kuwa hakuna uhakika wa kufanikiwa katika mjadala huo bali alisisitiza kuwa Ugiriki imeonesha kuwa na nia ya kutatua tatizo hilo hivyo haitakuwa sawa kutowapa nafasi nyingine ili waweza kurekebisha makosa yao na kuanza upya.