Spika wa Congress Brazil kushtakiwa

Haki miliki ya picha Alex Ferreira l Ag. Camara
Image caption Spika wa Congress,Eduardo Cunha

Waendesha mashtaka nchini Brazil wamefungua mashtaka ya rushwa na usafishaji wa fedha chafu dhidi ya spika wa congress, Eduardo Cunha.

Cunha anatuhumiwa kupokea dola milioni tano kama rushwa ili kuingia katika mikabata na shirika la mafuta la serikali, Petrobras.Bwana Cunha amekana tuhuma hizo na kusema zina ushawishi wa kisiasa.

Cunha ni mkosoaji mkubwa wa serikali ya rais Dilma Rousseff. Mashtaka pia yamefunguliwa dhidi ya aliyekuwa rais wa Brazil Fernando Collor de Mello, ambae pia amekana kufanya kosa lolote.

Idadi kubwa ya wanasiasa, wafanya biashara na watumishi wa umma wamefunguliwa mashtaka kuhusiana na sakata hilo la Petrobras katika kipindi cha mwaka mmoja.

Waandamanaji wanaopinga rushwa wamekusanyika katika ofisi ya wizara ya fedha mjini Rio de Janeiro kuonyesha hasira zao kwa kile walichokiita ukiukwaji wa demokrasia.