Dondoo za Beijing na John Nene

Image caption Uwanja wa birds nest utakaoumiwa kwa michezo hiyo

Mjini Beijing kuna vyakula mbali mbali lakini kwa wenzangu kutoka bara la Afrika ambao wamezoea ugali, fufu na vyakula vingine vizito vya kushibisha hapa wameambulia patupu.

Hivyo basi rafiki yangu kutoka Nigeria (jina lake nitalibana) ameamua kushiba kabisa wakati wa kiamsha kinywa, akisema vyakula vya China ni vyepesi mno havimshibishi kama alivyozoea kule nyumbani.

Image caption Beijing

Mayai anakula karibu kumi kila asubuhi pamoja na sausage tano, nusu mkate huku nusu nyingine anaibeba na mayai ya kuchemsha pia ili kujaza pengo la chakula cha mchana. Zaidi hapa wali waliwa sana na kuku, nyama na ukipenda pia mbwa wapo. '' ''Nimechoshwa na vyakula vya hapa, ni kama maji, sasa nitakua najaza kabisa asubuhi niweze kujimudu vilivyo,'' asema mwenzangu huyo wa Nigeria.

Na isitoshe, ana mfuko wake maalum wa kubeba matunda baada ya kiamsha kinywa. Utadhani ana biashara yake hapa Beijing ya kuuza matunda lakini yote hayo ni kwa sababu ya tumbo.

Image caption Bejing

Hapa hamna nyama choma ama ugali lakini kwangu mimi nimeamua kuishi jinsi watakavyo wao. Ukiwa Roma utafanya kama wa Roma ndio muelewane zaidi. Kama ni wali ndio hivyo nala lakini shingo upande maanake umechemshwa tu wala hauna ladha, ila pilipili ukitaka ipo kwa wingi.

Wakuu wa michezo kadhaa kutoka Afrika niliozungumza nao wameamua kula kuku tu, na hawataonja nyama nyingine wakiogopa kula mbwa. Hatahivyo kuna sehemu za nyama ya mbwa sio kote Beijing.

Mwanafunzi kutoka Uganda Stephen Kizito asema:''Mwana, mimi nakwisha choka kabisa na hii mchele kila siku..hakuna matoke hapa..mimi naumia sana lakini nitavumilia tu mpaka nirudi nyumbani.''

Image caption Bejing

Je, amejishindia mchumba kama baadhi ya wenzangu wengine kutoka Afrika Mashariki?,

Kizito anasema hajafurahishwa na kina dada wa China.

''Hao iko flat kabisa huku nyuma si kama wa kule kwetu. Mi napenda wetu wa nyumbani.Hao iko mzuri zaidi kuliko hawa lakini uzuri yao iko na roho mzuri nakaribisha mimi hapa kwa furaha.''

Haki miliki ya picha b
Image caption Bejing

Kutokana na ukosefu wa mafunzo ya bara la Afrika, hapa Afrika inajulikana kama Fei Zhou kwa Kichina yaani bara lisilo na mwanzaga.

Kuna baadhi yao wanafikiria Afrika ni taifa moja kwani utasikia wanakuuliza kama watoka taifa la Afrika, sehemu ambayo watu hulala mbugani.

Hatahivyo makosa si yao bali ya serikali kwa sababu wamefungiwa mitandao kadhaa ya kijamii kama vile Facebook, Twitter na Instagram. Wana mitandao yao ya hapa hapa lakini hawana habari zaidi kinachoendelea kwengine duniani. Ndio China hiyo.