Ghana:Mgomo wa madaktari wamaliza wiki 3

Image caption Mgomo wa madaktari Ghana

Nchini Ghana madaktari wamekuwa katika mgomo wa tangu wiki 3 zilizopita. Hospitali ya mjini Kumasi, mojawapo ya hospitali kuu nchini Ghana sasa imekuwa kama mahame, wengi wa wagonjwa wakilazimika kurudi makwao.

Kwa upande wao hospitali za kibinafsi na zile zinazomilikiwa na taasisi za kidini kama kanisa zimezidiwa na kazi kutokana na wingi wa wagonjwa kama hali inavyoonekana katika hospitali hii ya kanisa la Seventh Day Adventist la mjini Kumasi.

Kiongozi wa timu ya utawala wa hospitali, Solomon Baajobo, amesema sasa wanaishiwa na dawa kwa sababu ya ongezeko hilo la ghalfa la wagonjwa.

" Hata mda wa kawaida tunaoutumia kuwaona wagonjwa wetu sasa unapungua, lakini twajitahidi viwango vya ubora wa matibabu yetu visishuke " bwana. Baajobo ameongezea kusema .

Jumatatu wahusika watajaribu kufufua upya majadiliano kati ya serikali na madaktari baada ya mazungumzo ya awali kusambaratika kabisa mapema wiki hii.