Muhubiri wa Kenya aachiliwa kwa dhamana

Image caption Muhubiri Nganga

Muhubiri mwenye utata James Ng'ang'a ameachiliwa kwa dhama ya 500,000.

Amekuwa chini ya kizuizi cha polisi kwa siku mbili na ameshtakiwa na shtaka la kusababisha kifo kupitia uendeshaji gari mbaya.Shtaka ambalo amekanusha.

Muhubiri huyo pia amekana madai kwamba alijaribu kuficha kwamba ni yeye ndiye aliyekuwa dereva wakati gari hilo lilipogongana ana kwa ana na gari jingine na kumuua mwanamke mnamo mwezi Julai.

Kampeni katika mtandao wa twitter iliwashinikiza maafisa wa polisi kuchunguza ajali hiyo na kwa sasa jina lake linaendelea kusambaa katika mitndao ya kijamii.

Washtakiwa wenzake wakiwemo maafisa wawili wa polisi na mtu aliyejitokeza na kusema yeye ndiye aliyeendesha gari hilo pia waliwachiliwa kwa dhamana na mahakama hiyo ya Limuru.

Magazeti ya Kenya pia yameripoti kwamba nyumba ya muhubiri huyo iliopo katika mji wa Nairobi huko Karen imevamiwa na kulingana na gazeti la Standard , wezi walitoweka na vifaa vya kielektroniki na mali nyengine isiojulikana thamani yake.