Tamasha la muziki la busara laahirishwa

Image caption Sauti za busara

Tamasha maarufu la muziki huko Zanzibar, Sauti za busara halitafanyika mwaka kesho kwa kile kilichotajwa kuwa sababu za ukosefu wa fedha za kutosha.

Sauti za Busara, ni tamasha la kimataifa ambalo hufanyika mwezi wa pili kila mwaka na huvutia mashabiki wengi tangu ilipoanzishwa miaka 12 iliyopita,

''Tulikuwa na lengo la kukusanya angalau dola $200,000 kabla Julai, kwa ajili ya uandalizi wa '' Sauti za Busara 2016, lakini mpaka sasa tumeweza kupata dola $42,000 tu."alifafanua mmoja wa waandalizi wa tamasha hilo la muziki bwana Yusuf Mahmoud.

Zaidi ya hayo Yusuf Mahmoud ameongeza kusema ingawaje shughuli ya uuzwaji wa tikiti za kiingilio kwa tamasha la Sauti za Busara haijakumbwa na matatizo yoyote ,lakini shida ni kuwa fedha inayopatikana ni asilimia 30% tu gharama za uaandaaji wa tamasha lenyewe.