Waliom'baka na kumuua msichana wasakwa

Image caption Waomboleza

Serikali ya Sierra Leone imetangaza kuwa itampa kitita cha dola $1,000 (£640) zawadi mtu yeyote atakaye toa habari zitakazofanikisha kukamatwa kwa genge linalotuhumiwa kum'baka na kumuua msichana aliyekuwa chini ya miaka 18.

Mwili wa msichana Hannah Bockarie, anayesemekana alikuwa akifanya kazi ya uchangu doa ulipatikana ufuoni mwa bahari ya eneo la mji mkuu wa nchi hiyo , Freetown, huku akiwa amejazwa michanga mdomoni mwake.

Jana usiku wanawake wanaotetea haki za binadamu walikusanyika na kuwasha mishumaa wakiomboleza kifo chake.

Wengi wameshtushwa na jinsi alivyouawa kikatili kama picha zilizotandazwa mitandaoni zilivyodhihirisha.

Wanaharakati hao sasa wameanzisha kampeni ya kukemea kitendo hicho na kutaka wahalifu hao kuchukuliwa hatua za kisheria, kampeni hiyo wameipa jina 'mimi ni Hannah".