Ufaransa yawasifu Wamarekani

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ufaransa yawasifu Wamarekani

Waziri wa masuala ya ndami wa Ufaransa Bernard Cazeneuve, amesifu ujasiri wa abiria watatu raia wa Marekani ambao walimshinda mwanamme ambaye alikuwa amejihami vikali aliyekuwa ndani ya treni ya kusafiri kwa mwendo wa kasi kati ya Amsterdan na Paris.

Mwananme huyo mwenye asili ya Morocco alikuwa na bunduki, bastola na kisu

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ufaransa yawasifu Wamarekani

Waamerika hao wawili kati ambao kati yao walikuwa wanajeshi waliokuwa likizoni walimkabili mtu huyo alipokuwa akitaka kumfyatulia risisi mfanyikazi mmoja wa treni.

Mmoja wa waamerika hao alichomwa kisu na abiria mwingine akapigwa risasi na wote wako hospitalini.

Polisi wa kupambana ugaidi wa ufaransa wanaendelea na uchunguzi. Utawala chini Ufarsana na Marekani unasema kuwa abiria hao walizuia kile walichokitaja kuwa kisa kibaya,