Mtu mwenye silaha akamatwa Ufaransa

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mtu mwenye silaha akamatwa Ufaransa

Mtu aliyekuwa amejihami vikali ameshindwa nguvu na abiria kwenye treni moja ya mwendo wa kasi iliyokuwa safarini kutoka Amsterdam kwenda Paris.

Mtu huyo mwenye umri wa miaka 26 raia wa Morocco aliripotiwa kuwa na bunduki ya rashasha, bastola na kisu.

Alikabiliwa na abiria wakiwemo raia watatu wa marekani wawili wakiwemo wanajeshi waliokuwa likizoni.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mtu mwenye silaha akamatwa Ufaransa

Mmoja wa waamerika hao alichomwa kisu na abiria mwingine akapigwa risasi na wote wako hospitalini.

Polisi wa kupambana ugaidi wa Ufaransa wanaendelea na uchunguzi. Utawala chini Ufaransa na Marekani unasema kuwa abiria hao walizuia kile walichokitaja kuwa kisa kibaya,