9 wauawa kwenye shambulizi Somalia

Haki miliki ya picha AP
Image caption 9 wauawa kwenye shambulizi Somalia

Shambulizi la kujitoa mhanga kusini mwa somalia limewaua takriban watu 9 katika kituo kimoja cha kutoa mafunzo ya kijeshi.

Gari lililokuwa limejazwa milipuko lililipuka katika mji wa bandari wa kismayo.

Jeshi la kulinda amani la umoja wa mataifa linasema kuwa washambuliaji wawili waliuawa.

Wanajeshi kadha wa AU pia ni kati ya wale waliojeruhiwa. Mji wa Kismayo ni moja ya ngome za kundi la kiislamu la al shabab.