Korea zote mbili zaanza mazungumzo

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Korea zote mbili zaanza mazungumzo

Mazungumzo kati ya Korea Kaskazini na kusini kujaribu kuzuia makabaliano eneo la mpaka yamerejelewa tena.

Mazungumzo hayo yalihairishwa baada ya kuendelea hadi Jumamosi usiku. Hakuna taarifa zozote zilizoibuka kutoka kwa mazungumzo hayo.

Lakini mwandishi wa BBC mjini Seoul anasema kuwa sababu kuwa mazungumzo hayo yalichukua saa nyingi, kuna matumaini kuwa hali iliyo sasa inaweza kutatuliwa.

Walikubaliana kafanya mazungumzo muda mfupi kabla ya muda wa mwisho uliokuwa umetangazwa na Korea Kaskazini wa kutaka matangazo ya propaganda kutoka Korea Kusini kuzimwa.