AI:Upinzani unanyanyaswa Burundi

Haki miliki ya picha
Image caption Burundi

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu , Amnesty International,linasema kuwa maafisa wa usalama nchini Burundi wametumia vyuma na tindikali kushambulia watu wanaoshukiwa kuunga mkono upinzani wakati wa kampeni za hivi karibuni za kuelekea uchaguzi wa Urais.

Ushahidi ulioandikwa katika ripoti hiyo ya Amnesty unashtumu polisi na maafisa wa idara ya ujasusi kwa kuwakamata watu kinyume cha sheria na kulazimisha washukiwa kukiri makosa.

Hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kugombea muhula wa tatu ilishtumiwa na upinzani na kutajwa kama ukiukaji wa katiba ya nchi hiyo.

Maandamano yamekuwa yakifanyika nchini humo kwa miezi kadhaa kupinga uamuzi huo.

Shirika la Amnesty linasema watu wote waliozuiliwa hawakupewa fursa ya kupata uakilishi wa kisheria.