Vikwazo dhidi ya Iran kuondolewa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hammond na Zarif

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza amesema huenda vikwazo dhidi ya Iran vikaanza kuondolewa mapema mwaka ujao.

Philip Hammond yuko mjini Tehran kwa ufunguzi wa ubalozi wa Uingereza nchini humo na amefanya mazungumzo na rais wa Iran , Hassan Rouhani.

Bw Hammond amesema anaamini Iran ina nia ya kufungua ukurasa mpya katika kuimarisha uhusiano kati yake na nchi za magharibi.

Amesema kuwa Uingereza itashirikiana na Iran kukabiliana na tishio la kundi la kigaidi la ISIS.