Kenya:Walimu kupewa nyongeza ya asilimia 60

Image caption Walimu nchini Kenya wakifanya maandamano

Walimu nchini Kenya wana kila la wanatarajiwa kupokea nyongeza ya mshahara kwa hadi asilimia 60.

Mahakama ya juu imetoa uamuzi huo baada ya mvutano wa muda mrefu kati ya serikali na muungano wa walimu.

Serikali imekuwa ikisema haina uwezo wa kuendelea kuwapa nyongeza zaidi walimu laki mbili nchini humo.

Walimu walikuwa wameapa kugoma iwapo hawangepata nyongeza hiyo.