Umoja wa Ulaya na tatizo la wahamiaji

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kansela wa Ujerumani na Rais wa Ufaransa

Viongozi wa Ufaransa na Ujerumani wamezitaka nchi za Umoja wa Ulaya kufanya kazi pamoja kuweza kukabiliana na tatizo la wahamiaji.

Katika taarifa yao ya pamoja kwa vyombo vya habari mjini Berlin, Kansela Angela Merkel amesema kanuni zilizokuwepo sasa kama vile kuwasajili wahamiaji, hazifuatwi.

Kwa upande wake Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametaka mgawanyo sawa wa wanaoomba hifadhi, kati ya mataifa wanachama.