Mlipuaji awauwa watu 6 Nigeria

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mlipuko wa bomu Nigeria

Ripoti kutoka Nigeria zinasema mshambuliaji wa kike ya kutolea mhanga ameshambulia kituo kikuu cha basi katika mji wa Kaskazini Mashariki wa Damaturu na kusababisha mauaji ya watu sita.

Watu wengine ishirini na watano walijeruhiwa.

Walioshuhudia wanasema msichana huyo alikatazwa kuingia katika kituo hicho kabla ya kujilipua karibu na gari lililokuwa likipita na kuwaua waliokuwa ndani yake.