Hisa za China zazidi kuporomoka

Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Kushuka kwa hisa kumezidisha wasiwasi miongoni mwa wawekezaji

Jaribio la benki kuu nchini China ya kudhibiti soko la hisa la nchi hiyo limeshindwa kuzuia hasara zaidi.

Benki hiyo ilipunguza riba siku ya Jumane ili kupiga jeki ukopeshaji.

Lakini hata hivyo mauzo ya hisa mjini shangai yalifunga siku kwa kushuka kwa asilimia tatu.

Haki miliki ya picha
Image caption Jitihada za kuiimarisha hali zinaonekana kuto fuwa dafu

Hisa zilipanda nchini Japan, korea kusini na Taiwan lakini zikashuka chini New Zealand na Indonesia.

Kumekuwa na ongezeko la mauzo katika masoko ya hisa nchini china siku moja baada ya benki kuu kupunguza riba ili koungezesha ukopeshaji kwa lengo la kuzipiga jeki bei za hisa.

Masoko ya hisa mjini Shangai yalipanda kwa asilimia 0.8 baada ya kushuka saa za asubuhi.

Hisa mjini Tokyo nchini Japan zilipanda kwa zaidi ya asilimia moja lakini mauzo katika masoko mengine barani Asia yalishuka.