Macho yote yaelekezwa Sudan Kusini

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Kiir (kushoto) hakutia saini makubaliano yaliosainiwa na Riek Machar

Rais Kiir anatarajiwa kutia saini makubaliano Jumatano licha ya kwamba msemaji wake anasema bado hakubaliani na baadhi ya yaliomo.

Kiongozi wa upinzani Riek Machar alikubali masharti ya makubaliano hayo na kuyatia saini wiki iliyopita.

Mapigano kati ya vikosi vinavyowatii Rais Kiir na Riek Machar yamesababisha watu milioni 2.2 kupoteza makaazi yao.

Haki miliki ya picha
Image caption Wakaazi wengi wamepoteza makaazi yao kutokana na vita Sudan kusini

Katika mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa, mkuu wa misaada, Stephen O'Brien ameonya kwamba hali inazidi kuwa mbaya akieleza kwamba amepokea visa vya uovu uliofanywa ikiwemo watu kuteketezewa moto nyumba zao.

"Ukubwa na kiwango cha uovu uliogubika mashambulio dhidi ya raia unaashiria uzito unaopita tofuati za kisiasa," alisema.

Image caption Mapigano yamekuwa yakiendelea licha ya jitihada za kuleta amani

Baadaye, rais wa sasa wa baraza hilo la usalama, Balozi wa Nigeria Joy Ogwu, amesema baraza hilo limeungana kuhusu hali Sudan kusini.

"Sote tunakubaliana kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa kwa yoyote atakayepatikana na makosa atawajibishwa," alisema.

Rasimu ya azimio la Marekani itaidhinisha marufuku ya uuzaji wa silaha kwa nchi hiyo, pamoja na kuidhnishwa vikwazo vingine iwapo rais Kiir hatotia saini makubaliano hayo.

Sudan kusini ni nchi changa duniani, iliyojtangaza uhuru wake mnamo 2011.