Makamanda wa Iraq wauawa na waasi wa I-S

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Shambulio la Bomu Iraq

Makamanda wawili wa ngazi ya juu katika jeshi la Iraq wameuawa katika shambulio la bomu lililotegwa ndani ya gari.

Shambulio hilo limefanyika katika mji wa Ramaddi ambapo serikali inapamabana na wanamgambo wa Islamic State.

Mmoja wa maafisa hao alikua naibu kamanda anayeongoza harakati za kijeshi katika eneo hilo.

Eneo la Ramadi lilitekwa na wapiganaji wa I-S mnamo mwezi May, hatua ambayo wachambuzi wanasema ni pigo kubwa kwa serikali.

Harakati za jeshi kulikomboa eneo hilo hazionekani kufaulu na huemnda mauaji ya makamanda hao yakawavunja moyo zaidi.