Wahamiaji zaidi ya 50 wafariki Libya

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wahamiaji wanajaribu kwenda Ulaya

Watu wapatao 50 wamekutwa wamekufa katika sehemu ya mizigo ya boti iliyokuwa imebeba wahamiaji waliokamatwa katika pwani ya Libya.

Vyombo vya habari vya Italia vimesem kwamba vifo hivyo vinaweza kuwa vimesababishwa na kukosa hewa.

Kiasi cha watu 430 waliokolewa wakiwa hai kutoka katika boti hiyo na boti ya ulinzi ya Sweden.

Maelfu ya wahamiaji wamekufa na maelfu wengine kuokolewa baada ya kurundikwa katika meli moja hivi karibuni huko Libya.

Zoezi la uokoaji katika moja mazoezi kumi ya aina lilifanyika katika bahari nchini Libya,Alisema mlinzi mmoja wa pwani ya Italia.

Mapema mwezi Agosti,Kikosi cha wanamaji cha Italia kiligundua miili ya watu arobaini na tisa katika meli moja.

Wahamiaji hao wanadaiwa kufariki kutokana na kukosa hewa.

Wahanga wa tukio hilo walisema kuwa walilazimishwa kubaki katika chombo hicho ambacho kilijaa kupita kiasi.

Wasafirishaji haramu waliopo nchini Libya,wanaaminika kutengeneza faida kubwa kwa kuwasafirisha wahamiaji mpaka mwambao wa Ulaya.

Maafisa wa Ulaya wameelezea hatma ya wahamiaji, karibia 250,000 ambao wamesaifiri kwa mashua mpaka ulaya kama wengi kupitiliza makadirio.

Umoja wa mataifa umesema kuwa kwa mwaka huu pekee, zaidi ya wahamiaji 2,000 wamefariki dunia walipokuwa wakijaribu kuvuka bahari na kwenda ulaya.

Wakati huo huo suala la uhamiaji linatarajiwa kutawala mkutano wa kilele mjini Vienna na kuhudhuriwa na viongozi kutoka Ujerumani, Austria na nchi za Balkan .

Kuelekea mkutano huo waziri wa mambo ya kigeni wa Austria Sebastian Kurz ameiambia BBC kuwa sheria za umoja wa ulaya kuhusu uhamiaji hazina nguvu. Alieleza kushindwa kwa kanuni za Dublin ambazo ziliwataka wahamiaji kutoka nje ya ulaya kujisajili kwenye nchi za awali wanazofikia.

Mapema wiki hii Polisi wa Macedonia walitumia mabomu ya machozi baada ya maelfu ya wahamiaji kuvuka kwa nguvu kwenye kizuizi kilichowekwa na polisi katika mpaka wa Ugiriki.