Muuaji ajiua Marekani

Image caption Mauaji Marekani

Polisi nchini Marekani imesema muuaji wa Waandishi wawili wa habari nchini Marekani amefariki.

Ujumbe unaoonekana kutumwa na mtu aliyekuwa na silaha nchini Marekani na kuwaua kwa risasi watangazaji hao wawili wa televisheni wakati wa matangazo ya moja kwa moja unaashiria kwamba alikuwa na uchungu kwa kinachoonekana kuwa ubaguzi wa rangi.

Vester Lee Flanagan, aliyefutwa kazi katika kituo hicho cha televisheni alifariki baada ya kujipiga risasi, saa chache baadaye.

Msimaizi wa kituo hicho cha televisheni alimtaja mshambuliaji huyo kuwa mtu asiyekuwa na furaha ambaye ilikuwa vigumu kufanya naye kazi.