Nkurunziza atoa wito kupambana na mauaji

Haki miliki ya picha
Image caption Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi

Katika hotuba kwa taifa rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza ameonyesha hisia zake kuhusu kujumuisha vikosi vya usalama nchini humo.

Hayo yamekuja wiki moja baada ya kuapishwa kushika hatamu za uongozi wa nchi hiyo ambapo wakasoaji wanasema ni kinyume cha katiba.

Suala hilo limezusha ghasia kali na jaribio lililotibuka la kuipindua serikali.

Amezitaka kamati za usalama kufanya kazi usiku na mchana kupambana kile alichokiita kundi la watu wachache wanaofanya mauaji na kusababisha hofu kwa raia.

Amesema vijana hasa wa vyuo vikuu sasa watapata mafunzo ya uzalendo.