Mwanaharakati afikisha mahakamani Uchina

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Joshua Wong

Kiongozi wa maandamano ya mwaka jana ya kuunga mkono demokrasia nchini Hong Kong ameshtakiwa kwa makosa ya kukusanyika kiharamu.

Mwanaharakati huyo Joshua Wong, huedna akakabiliwa na kifungo cha hadi miaka mitano gerezani.

Mwanaharakati huyo anakiri kuuzunguka ukuta wa chuma unaozunguka makao makuu ya serikali mnamo Septemba mwaka jana.

Lakini anakana kwamba alifanya chochote kinyume cha sheria.

Picha zilizomuonyesha akibururwa na polisi huku akipiga mateke na kupiga kelele zilisabaisha maelfu ya watu kuandamana barabarani na kuidhinisha kilichokuja kujulikana kama Umbrella Movement, maandamano dhidi ya mpango wa serikali ya ya Uchina kuhusu mageuzi ya kisiasa Hong Kong.

Wakati polisi ilipoutawanya umati kwa kutumia gesi ya kutoa machozi, waandamanji zaidi waliwasili na kusababisha kuanza kwa vuguvugu hilo.

Wakili wake, Michael Vidler, anasema mashtaka yanayomkabili muda mrefu baada ya kukamtwa kwake yamechochewa kisias