Maelfu waachwa bila makao DRC

Haki miliki ya picha RIA Novosti
Image caption Moto ukiteketeza msitu

Maelfu ya watu nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameachwa bila makao baada ya moto kuharibu nyumba zao, katika mkoa wa Maniema Mashariki mwa nchi hiyo.

Ripoti zinasema moto huo umeteketeza maelfu ya ekari ya misitu na upepo mkali unaovuma, unafanya moto huo kusambaa kwa haraka.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Sokwe katika msitu mmoja nchini Congo

Shirika la kutoa misaada ya kibinadam la Umoja wa Mataifa, UNOCHA, limesema kuwa katika wilaya ya Kabambare zaidi ya nyumba mia tatu zimeteketea, katika vijiji vitatu.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa nchini humo, amesema kuwa kuna uwezekano wa baadhi ya mioto hiyo kuanzisha kimakusudi na makundi ya waasi yaliyojihami.