Maelfu waandamana Malaysia

Image caption Maelfu wandamana Kuala Lumpur

Maelfu ya waandamaji wanaopinga serikali wamekusanyika katika nji mkuu wa Malaysia, Kuala Lumpur wakitaka waziri mkuu Najib Razak ajiuzulu kwa madai ya ufisadi yanayomkabili.

Mkutano huu wa hadhara umekuwa ukiendelea kwa siku mbili sasa hata baada ya polisi kuupiga marufuku.

Waandamanaji hao pia walikiuka amri rasmi ya kutovaa nguo za manjano zinazotumika na kundi ambalo limeandaa maandamano hayo.

maandamano hayo yalianzishwa baada ya zaidi ya dola milioni mia moja kupatikana katika akaunti ya kibinafsi ya waziri mkuu. Amesisitiza kuwa pesa hizo zilikuwa za msaada na akakanusha kufanya kosa lolote.