Usitishwaji vita watangazwa Sudan.K

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Riek Machar

Kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini Riek Machar ametangaza usitishwaji vita wa kudumu kuanzia usiku wa manane hii leo Jumamosi . Bwana Machar na rais Salva Kiirr walitia sahihi makubaliano ya amani mapema mwezi huu ambapo iliafikiwa kuwa usitishwaji mapigano utafuatia.

Rais Kiir naye pia ametoa wito akilitaka jeshi lake liache kupigana.

Kumekuwa na mapigano katika maeneo yayouzunguka mji wa Bentiu siku chache zilizopita.

Mapigano kati ya vikosi watiifu kwa wawili hao yamesababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwalazimisha watu zaidi ya milioni mbili kuhama makwao.