Maandamano yaingia siku ya 2 Malaysia

Haki miliki ya picha PUSPAWATI ROSMAN
Image caption Waandamanaji mjini Kuala Lumpur

Maelfu ya watu wanashiriki katika siku ya pili ya maandamano ya kupinga serikali kwenye mji mkuu wa Malaysia Kuala Lumpur.

Mamia walikesha kwenye mitaa usiku kucha. Polisi wametangaza maandamano hayo kuwa haramu lakini hawajachukua hatua za kuyavunja.

Pia kumekuwa na maandamano katika miji mingine ya nchi hiyo lakini yamekwisha..

Haki miliki ya picha
Image caption Waziri mkuu Najib Razak

Wanaharakati nchini humo wanataka waziri mkuu nchini Malaysia Najib Razak ajiuzulu.

Wanaamini kuwa hajaelezwa vilivyo ni kwani nini akaunti zake ya benki zilipataika zikiwa na mamilioni ya dola.