Mshukiwa wa ugaidi ashtakiwa Bangkok

Haki miliki ya picha THAI ROYAL POLICE
Image caption Mshukiwa wa ugaidi Bangkok

Mtu aliyekamatwa kuhusiana na mlipuko wa bomu uliotokea mjini Bangkok nchini Thailand ameshtakiwa kwa kosa la kupatikana na silaha.

Polisi wanaamini kuwa mtu huyo mwenye umri wa miaka 28 alihusika na mlipuko uliotokea mjini humo majuma mawili yaliyopita.

Maafisa sasa wamepanua shughuli zao za kuwasaka washukiwa zaidi. Taarifa moja ya vyombo vya habari ilimunukuu msemaji wa polisi akisema kuwa mtu huyo aliye kuzuizini huenda akawa moja wa genge linalohusika na usafirishaji haramu wa binadamu.

Alikamatwa kwenye nyumba moja nje ya mji wa Bangkok jana Jumamosi.