Austria yaanzisha ukaguzi mkali mpakani

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Austria yaanzisha ukaguzi mkali mpakani

Austria imeanzisha hatua kali za ukaguzi katika eneo la mashariki la mpaka wake katika jaribio la kuzuia usafirishaji haramu wa watu.

Hatua hiyo imesababisha kuwepo kwa msongamano mkubwa wa magari wa urefu wa hadi kilmita 20 kweda nchini Hungary.

Wiki iliyopita utawala nchini Austria uligundua miili ya wakimbizi 71 katika lori moja lililokuwa limetelekezwa ambalo lilikuwa limesafiri kutoka nchini Hungary.

Mapema serikali ya Hungary ilipinga shutuma baada ya kuweka ua kwenye mpaka wake na Serbia kuzuia wahamiaji.