Washukiwa 38 wa ugaidi wakamatwa TZ

Image caption Polisi Tanzania wakiwa kwenye mafunzo ya kupamabana na ugaidi

Polisi nchini Tanzania wanasema wamewakamata washukiwa 38 wa ugaidi ambao wanauhusiano na kundi la kigaidi lililofanya mashambulio katika vituo kadhaa vya polisi nchini humo.

Washukiwa hao walikamatwa wakiwa na bunduki kumi na risasi 387, mabomu ya kurushwa kwa mkono maarufu kama grunedi na vifaa vya kutengenezea mabomu.

Hata hivyo idara ya polisi nchini Tanzania, halijasema ni lini washukiwa hao walikamatwa au siku watakayofikishwa mahakamani.

Katika kikao na waandishi wa habari, mkuu wa polisi Suileman Kova, aliwaonyesha waandishi wa habari silaha walizonasa kutoka kwa washukiwa hao.

Amesema uchunguzi wa awali, umebainisha kuwa kuna uwezekano mkuwa kuwa waliokamatwa wana mitandao mingine ya kigaidi.

Image caption Ramani ya Tanzania

Amesema washukiwa hao walikamatwa baada ya operesheni kali iliyofanywa katika miji ya Lindi na Tanga.

Bila kutaja majina yao, Kova amesema kuwa miongoni mwa wa waliokama ni wavulana walio na umri wa chini ya miaka 17.

Kukamatwa kwa washukiwa hao kunajiri baada ya vituo vinne vya polisi kushambuliwa nchini Tanzania, tukio la hivi karibuni likiwa shambulio dhidi ya kituo cha Staki Shari mjini Dar e Salaam.

Julai 15, mwaka huu watu waliokuwa wamejihami walishambuio kituo cha polisi mji Dar es Salaam na kuwauawa maafisa saba wa polisi na raia kadhaa, kabla ya kutoweka na idadi ya silaha isiyojulikana.

Katika tukio lingine lililofanana na filamu, watu waliokuwa wamejihami walishambulia kituo cha polisi katika wilaya ya Bukombe, eneo la Geita na kuwauawa maafisa wawili wa polisi.