Misri yatangaza tarehe uchaguzi wa bunge

Haki miliki ya picha AP
Image caption Jengo la Bunge la Misri

Mamlaka ya uchaguzi nchini Misri imesema kuwa uchaguzi wa wabunge nchini humo unatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba na Novemba mwaka huu,ikiwa ni miaka mitatu tangu kufanyika kwa uchaguzi kama huo.

Bunge la Misri lililokuwa chini ya utawala wa Kiislam lilifikia ukomo wake mwaka 2012 mwaka mmoja tangu kuchaguliwa kwa Rais wa kwanza wa dola ya Kiislam Mohammed Morsi ambaye alipinduliwa na jeshi.

Mkuu wa tume ya uchaguzi ya Misri Ayman Abbas amesema kuwa taratibu za uchaguzi huo zitafanyika katika majimbo yote ya uchaguzi jumamosi na jumapili ya Oktoba 17 na 18 mwaka 2015

Hata hivyo akizungumzia uchaguzi wa ndani amesema kuwa utafanyika Oktoba siku ya Jumapili na Jumatatu ya Oktoba 18 na 19