Mzozo waibuka kati ya Hungary , Ufaransa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mzozo waibuka kati ya Hungary , Ufaransa

Mzozo wa kidiplomasia umeibuka kati ya Hungary na Ufaransa juu ya uamuzi wa Hungary kuezeka ua nyembamba katika mpaka wake na Serbia ili kuzuia kuingia wahamiaji haramu.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius amesema kuwa ujenzi wa ua huo ni ukiukaji wa maadili ya nchi za ulaya. Lakini mwenzaeke kutoka upande wa Hungary Peter Szijjarto ameelezea kushangazwa kwake na madai hayo.

Image caption Mzozo waibuka kati ya Hungary , Ufaransa

Amesema kuwa bara Ulaya linastahili kushirikiana kukabiliana na tatizo la uhamiaji haramu badala ya kuelekezeana lawama.

Bwana Szijjarto amesema kuwa amemuita balozi wa Ufaransa nchini Hungary kuja kueleza madai hayo ya Ufaransa. Inadaiwa kuwa zaidi ya wahamiaji haramu elfu hamsini wameingia nchini Hungary katika mwezi Agosti pekee.