Razak akataa kujiuzulu

Haki miliki ya picha AP
Image caption Najib Razak

Waziri mkuu wa Malaysia , Najib Razak, amepinga wito wa kujiuzulu kwake kufuatia madai ya ufisadi.

Katika hotuba yake kuadhimisha siku ya ukombozi wa Malaysia bwana Najib amesema kuwa maandamano ya kumtaka ajiuzulu sio njia muafaka ya kuelezea tetesi zao.

Haki miliki ya picha GETTY IMAGES
Image caption Waandamanaji nchini Malaysia

Maelfu ya waandamanaji wamekuwa wakifurika barabara za mji mkuu mwishoni mwa wiki wakimtaka ajiuzulu kwa madai kuwa alifuja mamilio ya fedha za umma.

Waziri mkuu huyo amekanusha madai hayo yote.