EU wajipanga kudhibiti wahamiaji

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wahamiaji wakiokolewa katika usafiri wa majini wakati wakielekea Ulaya

Jumuiya ya Ulaya EU imetangaza mkutano wa dharula wa Mawaziri wake wa Mambo ya nje wenye lengo la kujadili mbinu za kukabiliana na ongezeko la wahamiaji ambao unatarajiwa kufanyika ndani ya wiki mbili Septemba 14 mwaka huu.

Kauli hiyo kuhusiana na mkutano huo imetolewa Luxembourg,Ujerumani nchi ambayo kwa sasa ndiyo inayoshikilia nafasi ya Urais wa Jumuiya hiyo nafasi ambao wamekuwa wakipongezana miongoni mwa nchi wanachama.

Ripoti hiyo imesisitiza kuwa hali ya wahamiaji kwa sasa ni mbaya na inahitaji hatua za haraka ili kukabiliana na ongezeko kubwa la wahamiaji.

Uingereza,Ufaransa na Ujeruman wamesema kuna haja ya wahamiaji kuchukuliwa alama za vidole na kusajiliwa wakati wanaingia Italia na Ugiriki.

Hata hivyo nchi wanachama wa jumuiya hiyo ya Ulaya EU wamesema kuwa wataanzisha orodha ya nchi zenye asili ya usalama na kuruhusu kurejeshwa nchini kwao baadhi ya wahamiaji hao.

Mapema Waziri wa mamabo ya kigeni wa Ufaransa Laurent Fabius, amezilaumu baadhi ya nchi wanachama wa EU kwa kukataa kuwachukua wakimbizi katika nchi zao.