Machar ashutumu jeshi la serikali

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Riek Machar

Kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini amewashutumu wanajeshi wa serikali kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano saa chache baada ya kuanza kutekelezwa.

Riek Machar amesema kuwa jeshi la Sudan Kusini lilishambulia vikosi vyake katika majimbo ya Unity na Upper Nile, kaskazini mwa nchi.

Jeshi la serikali hata hivyo limekanusha madai hayo.

Maafikiano kadha ya kusitisha mapigano yameafikiwa, tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vianze karibu miaka miwili iliyopita.

Hata hivyo makubaliano hayo yalivunjika.