Maandamano yazuka nje ya bunge- Ukraine

Image caption Maandamano Ukraine

Afisa mmoja wa polisi ameuawa na wengine zaidi ya mia moja kujeruhiwa nje ya jengo la bunge la Ukraine, baada ya wabunge wa nchi hiyo kuunga mkono mpango wa awali wa kuipa eneo linalothibitiwa na waasi Mashariki mwa nchi hiyo, mamlaka ya kijitawala.

Waandamanaji waliwarushia mawe na mabomu ya petroli maafisa hao na kuna ripoti kuwa kulitokea mlipuko kati kati mwa waandamanaji hao.

Maandamano hayo yalitokea muda mfupi baada ya wabunge kuidhinisha eneo la Donetsk na Luhansk ambayo yamo chini ya waasi wanaoungwa mkono na Urussi mamlaka zaidi.

Mkataba wa amani wa kusitisha mapigano ungali unadumisha nchini humo.

Mkataba wa amani wavunjwa

Mpango huo ulioidhinishwa na wabunge na sehemu ya mkataba huo uliosainiwa mwezi Februari mjini Minsk.

Wakati huu wa msimu wa joto mapigano kati ya wanajeshi wa Ukraine na waasi yameongezeka.

Lakini pande hizo mbili ziliafikiana wiki iliyopita kusitisha mapigano hayo hiyo kesho, wakati wanafunzi watakapokuwa wakirejea shuleni.

Image caption Maandamano Ukraine

Licha ya kuwa mikataba kadhaa ya kusitisha mapigano yamekiukwa katika siku za hivi karibuni, afisa mmoja mwandamizi wa shirika la kimataifa la OSCE, nchini Ukraine, Alexander Hug, ameonya kuwa hakuna upande wowote katika mzozo huo umedumisha mkataba huo wa kusitishwa mapigano.

Lakini muda mfupi baada ya wabunge 265, kuidhisha mswada huo wa ugatuzi katika bunge la nchi hiyo, maandamano nje ya bunge yakachacha.