Watson, Ivanovic wachapwa US Open 2015

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mcheza Tenisi, Heather Watson

Muingereza Heather Watson amepoteza mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza katika michuano ya wazi ya Us Open.

Watson amepoteza mchezo huo mbele ya Mmarekani Lauren Davis kwa seti 7-6 (7-3) 7-6 (7-0).

Nyota huyu ambaye alishinda michuano ya vijana mwaka 2009 ameshindwa kushinda michezo yake ya kwanza toka mwaka 2011.

Nae nyota namba saba kwa ubora duniani Ana Ivanovic, wa Serbia alipoteza mchezo kwa Dominika Ciblukova wa Slovakia, kwa seti 6-3 3-6 6-3.