Kimbunga Fred kimepunguza kasi Cape Verde

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kisiwa cha Cape Verde

Kimbunga kikali chenye upepo wa kasi ya hadi kilomita 120 kwa saa kimekumba taifa la visiwa la Cape Verde, lililoko Afrika Magharibi.

Serikali nchini humo imesitisha safari zote za ndege huku mvua kubwa na upepo vikikabili visiwa vya Kaskazini-Magharibi vya taifa hilo.

Hakuna kimbunga kilichowahi kushuhudiwa katika eneo la Mashariki mwa bahari ya Atlantic inayokuwa na mvua nyingi.

Baadaye Jumatatu kimbunga hicho kwa jina Fred kilipunguza kasi na kuwa upepo wa kawaida kikielekea kupita visiwa hivyo, haya ni kwa mujibu wa kituo cha Kitaifa cha kuchunguza Vimbunga (NHC) kilicho na makao yake Marekani, kilisema.

Upepo mkubwa na mvua vinatarajiwa kuendelea huku kimbunga Fred kikipitia maeneo mengine ya Cape Verde siku ya Jumanne.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kimbunga Fred

Kituo hicho kilisema mara ya mwisho kimbunga kuwahi kupiga Cape Verde ilikuwa mwaka wa 1892, ingawa kimetahadharisha kuwa vitabu vya kumbukumbu havikuwa sahihi na ufasaha wa kutosha nyakati hizo kabla ya kuanza kwa mfumo wa kutumia mtambo wa satelite kuchunguza hali ya anga katikati mwa miaka ya 1960.

Cape Verde hujumuisha visiwa 10 vikubwa vya volkano, tisa ambavyo huishi watu.