Marekani na Viwanda bandia vya dawa

Haki miliki ya picha Science Photo Library
Image caption Dawa za binadamu,ambapo huko Marekani viwanda bandia vipo

Mamlaka nchini Marekani zimefanikiwa kuwakamata zaidi ya watu 90 na wamegundua na kuzifunga maabara 16 zilizokuwa chini ya ardhi kwa lengo la kutengeza dawa za binadamu kinyume cha sheria.

Mkuu wa kitengo cha madawa amesema kuwa kilo na maelfu ya ujazo wa kemikali yaliharibiwa katika miji majimbo 20 kufuatia msako wa miezi mitano.

Maofisa uchunguzi wa Marekani wanasema kuwa malighafi za kutengenezea dawa hizo inaingizwa nchini humo kutoka China.

Hata hivyo msako umeweza kubainisha na kushambulia magenge ya watengenezaji hao wa dawa mbandia chini ya ardhi